Mama Na Malezi Ya Mtoto

Kumtambuwa Muumba na kufuata maamrisho Yake ndicho kinachompa thamani mwanadamu. Afya, utulivu na furaha huja katika namna hiyo hiyo tunapotowa huduma kwa binadamu, tunapaswa kulenga kupata radhi za Allah Mtukufu.
Sisi kama wanawake vijana, tunajifunza kuhusu taji la kuwa mama kutoka ndani ya Qur’an na Sunnah. Kama ambavyo tunajifunza kila kitu kuhusu maisha, vivyo hivyo tunajifunza kuhusu malezi na kuwa mama kutoka ndani ya chanzo hicho hicho. Hivyo, baada ya kujua namna ya kuwa waja wa Allah Mtukufu, hatupaswi kuacha kumuomba msaada wakati tukiwalea watoto wetu.
Amani na Salamu ziwe juu ya mama wa Mtume wetu kipenzi(s.a.w) na wakeze, ambao ni mama zetu. Amani na salamu pia ziende kwa mama ambao walikufa kishahidi. Mwisho lakini sio kwa umuhimu, salamu maalumu ziende kwa yule ambaye alipitiya maumivu makali katika kuwa njia ya mimi kuja hapa duniani na akanilea kwa nguvu na jitihada kubwa, mama yangu wa thamani, Emine DEMIR. Kila watakaosoma kitabu hiki kwa upendo na hamasa wapate baraka za dua za mama zao na kuwaombea wengine kuwa mama wema. Amiin!!!.


Read In Other Languages

ARABIC
ENGLISH
FRENCH